TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 29 March 2012

Taarifa ya BANGONET


Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilayani Bagamoyo (BANGONET) umeomba serikali kutumia ruzuku ya mfuko wa jimbo kuchapisha na kusambaza  katiba kwa wananchi ili waweze kusoma na kuielewa kabla ya mchakato wa kutoa maoni.

 Ombi hilo limekuja baada ya kufanya mdahalo na wananchi katika majimbo ya Bagamoyo mjini Chalinze ambayo ilihudhuriwa na wananchi 473 ambapo iligundulika kuwa ni wananchi wachache takribani asilimia 10 kati ya asilimia 100 ndio wanaitambua katiba na kati ya hao asilimia 5 tu ndio wamewahi kuisoma katiba ya sasa.

 Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana Katibu Mtendaji wa Asasi hiyo Leonard Bamkuwia alisema Katiba zinapatikana katika duka la serikali lililopo Dar es Salaam kwa bei ya shilingi 5000 kila nakala 1 bei ambayo mwananchi wa kawaida hawawezi kuimudu na si rahisi kufika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta katiba

“Ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika kutoa maoni yao juu ya kuandika katiba mpya ni vema serikali ikachukua jukumu la kuchapisha nakala za katiba na kuzisambaza kwa wananchi mijini na vijijini,”.

Alifafanua kuwa mjadala ambao umekuwa ukiendelea Bungeni kuhusiana na katiba mpya ulitawaliwa na misingi ya kibinafsi na ushabiki wa vyama vya kisiasa pasipo kuzingatia masuala ya kitaifa.

Bamkuwia alisema maadili ya kitaifa na uzalendo vimetoweka na hivyo kuwa na matabaka ya walio nacho na wasionacho ambavyo vimepelekea watanzania kuitwa mafisadi, kukithiri kwa vitendo vya rushwa na mawaziri kuingiza wananchi katika mikataba mibovu isiyokuwa na maslahi ya kitaifa.

Pia, alisisitiza kuwa na sera au mfumo wan chi unaoeleweka na utakaofuatwa na marais wote bila kujali itikadi za vyama vyao wanavyotoka.

No comments:

Post a Comment