TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 29 May 2012

Ghasia za sababisha uharibifu wa mali Zanzibar

Tairi zinawaka moto katika njia moja kuu Zanzibar kufuatia ghasia zilizosababishwa na wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohamed Aboud, ametoa taarifa kuhusiana na ghasia akisema walosababisha uharibifu wa mali watachukuliwa hatua

Hali ya utulivu imeripotiwa katika kisiwa cha Unguja Jumapili usiku, kufuatia ghasia na uharibifu wa mali mwishoni mwa wiki baada ya maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho.

Hata hivyo kwa mujibu wa VOA inaripoti kwamba kuna vizuizi katika njia muhimu za kisiwa hicho na watu wamebaki nyumbani, na haijulikana hali itakuwa vipi siku ya Jumatatu watu wakirudi kazini

Ghasia zilizuka Jumamosi baada ya wanaharakati wa kundi hilo kutaka kushambulia makao makuu ya polisi kufwatia kukamatwa kwa imam wa msikiti wa Biziredi ambaye ni mmoja kati ya wa viongozi wa Uamsho, Sheik Mussa AliJuma.

Picha na stori ni kwa hisani ya VOA

No comments:

Post a Comment