MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shabani ‘Keisha’
ameitaka jamii kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) katika sekta
mbalimbali ikiwemo pesa za kununulia mafuta ya kupunguza vidonda na muwasho wa
ngozi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Keisha alisema walemavu
wa ngozi wanakumbana na changamoto
nyingi ikiwemo kuishi kwa wasiwasi kutokana na watu wenye imani za kishirikina
kudhani kwamba ngozi hiyo ni chachu ya kujipatia utajiri.
Alisema hata yeye amewahi kukabiliwa na changamoto nyingi katika
maisha yake kutokana na hali ya kuwa na ulemavu wa ngozi, hivyo ameitaka jamii
kuwasaidia albino katika elimu, ajira na kuwalinda dhidi ya wauaji.
Alisema vitendo vya unyanyasaji dhidi yao vinazidi kuongezeka,
licha ya serikali kudhibiti na kufanikisha azma yao na baadhi ya watu wenye
imani hizo walifikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua.
“Mwanzo, vyombo vya dola vililishughulikia jambo hili na
kulidhibiti kwa kiasi kikubwa lakini kwa sasa linajirudia na linazidi
kuongezeka siku hadi siku na serikali inashindwa kuchukua hatua kama zile za
awali” alisema Keisha.
Akizungumzia maisha yake ya awali alisema aliwahikuchukizwa
alipokuwa mtoto kutokana na baadhia ya watoto kumuita ‘Zeruzeru’ na alijiona
kama si mmoja kati ya watoto hao hadi kufikia hatua ya kumwambia mama yake
hataki kwenda shule.
No comments:
Post a Comment