TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 24 May 2012

Momba anajipanga kuachia 'mdundiko'

BAADA ya kutamba na wimbo wake wa ‘Mi sio sharobaro’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini,  Alli Momba 'Momba' anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mdundiko’ ambao amemshirikisha nyota wa muziki huo, Juma Kassimu 'Juma Nature'.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Momba alisema wimbo huo unatarajiwa kuwa tofauti na nyimbo nyingine alizowahi kuzifanya.
"Nimefanya vizuri sana katika wimbo huo kutokana na ubunifu ambao nimeufanya hali inayoashiria naweza kumfunika Juma Nature ambaye nimemshirikisha katika singo hiyo," alisema Momba.
Pia,  msanii huyo aliwaomba mashabiki wa muziki huo kumpa ushirikiano wa kutosha katika wimbo anaotarajia kuuachia wakati wowote kuanzia sasa, pamoja na kazi zake zijazo.
Mbali na kujiandaa kutaka kutoka na kibao hicho, Momba alishawahi tamba na vibao vyake kama vile Nikusabahi, Kabwela, ambavyo vilifanya vizuri na kumtambulisha katika tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment