TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 10 May 2012

OBAMA NA NDOA YA JINSIA MOJA


Rais  wa  Marekani  Barack Obama  anaunga  mkono  moja kwa moja ndoa za  watu  wa  jinsia  moja, akiwa  rais  wa kwanza  kufanya  hivyo  nchini  humo.  

Obama  amesema kuwa  alisita, kwa sehemu,  kuhusu  ndoa  za  watu  wa jinsia moja  kwasababu  alifikiri  kuwa  mahusiano  ya  watu wawili kwa mujibu wa sheria za kiraia yanatosha.

 Katika  mahojiano  ya  televisheni  katika  ikulu  ya Marekani ameeleza  kuwa alikuwa  na  shaka  kuhusiana na  ukweli  kwamba  watu  wengi  neno  ndoa  ni  jambo ambalo  linazusha  hisia  kali  za  kitamaduni  na  imani  za kidini.

 Obama amesema  kuwa  kwa  sasa  ni  muhimu  kwake binafsi  kujitokeza  na  kuthibitisha  kuwa   mahusiano  ya watu  wa  jinsia  moja  yanafaa  kufikia  kuwa  watu  hao wanaweza  kuoana.

Source: Dw

No comments:

Post a Comment