TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 21 May 2012

Timbulo atoa kibao kipya cha Samson na Delila



 NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo kaachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Samson na Delila  ambao umezungumzia zaidi mapenzi na jinsi ambavyo mwanamke ana nguvu katika ushawishi wa mapenzi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Timbulo alisema wimbo huo katengeneza tofauti na nyimbo zake nyingine kwa lengo la kuwapa ladha tofauti mashabiki wake. 

“Wimbo huu naamini utafanya vizuri zaidi na mashabiki wangu wataupenda kupita kiasi hivyo nawaomba wapenzi wangu waeendelee kunipa sapoti katika kazi zangu” alisema Timbulo. 

Alisema wimbo huo uko tofauti na nyimbo zake ambazo zimewahi kutamba kwani amewaletea mashabiki ujumbe ambao ameuandika yeye mwenyewe tofauti na zile za mwanzo ambapo ilisemekana ameiba kopi kutoka kwa msanii wa Cameroon wanaojulikana kama X Maleya na wimbo wao unaoiywa yelele

Mbali na wimbo huo, Timbulo alishawahi tamba na nyimbo zake kama Domo langu, na ‘wa leo wa kesho’ nyimbo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na luninga. 

Msanii huyo amewaahidi mashabiki wake kwamba kwa sasa atawaletea nyimbo ambazo sio za kopi tena kwani amejipanga mwaka huu kuwaletea nyimbo ambazo ni nzuri na zitakazowafurahisha.

No comments:

Post a Comment