TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 6 July 2012

Ban Ki Moon amteua Dk. Migiro kuwa mjumbe wake maalumKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Naibu Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya Ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika.

Katibu Mkuu Bw. Ban Ki Moon ameeleza kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake lakini amekuwa mwalimu wake na amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuenzi mchango wake mkubwa.

Amemuelezea Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa, ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.

Source. Mo blog

No comments:

Post a Comment