TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 23 July 2012

Haji azungumzia baba yake alivyolishwa sumuMsanii wa Muziki wa dansi wa bendi ya Twanga Pepeta Haji Ramadhani ameelezea kwa masikitiko makubwa jinsi ambavyo baba yake mzazi Mzee Ramadhani alivyofariki dunia baada ya kupewa sumu.

Akihojiwa katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na runinga ya EATV, Haji alisema Baba yake  alifariki muda mrefu kutokana na kupewa sumu, kutokana na sababu za kisiasa kwa vile alikuwa ni Mjumbe wa CCM katika ngazi ya Wilaya.

Alieleza kuwa hakuna aliyeshuhudia tukio, lakini ushahidi ulijulikana baada ya kufanyiwa uchunguzi hospitalini na ndipo kubainika alilishwa sumu.

Pamoja na hayo, haji alieleza jinsi ambavyo mke wake alivyopewa mimba nje ya ndoa na kudai kuwa ni kitendo ambacho kinamuumiza japokuwa kamwe hawezi kumwacha mke wake kwasababu anampenda.

Alisema aliogopa jamii itamuelewaje kwasababu tayari wazazi wa mke wake walifariki dunia na kumwacha mwanamke huyo mikononi mwake hivyo aliogopa pia kumwacha kwasababu angepata shida na watoto.

Haji ni baba wa watoto watatu lakini wawili alieleza kuwa walizaliwa nje ya ndoa kwa maana kwamba wakati yupo katika mihangaiko ya kutafuta maisha mke wake alibeba mimba nje kitendo ambacho kilimuumiza.

No comments:

Post a Comment