TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 4 July 2012

Kikundi cha Waislam Kenya kulinda makanisa


Viongozi wa Kiislam nchini Kenya wamekubaliana kuunda vikundi binafsi vya ulinzi ili kulinda makanisa kufuatia kushambuliwa siku ya Jumapili.

Kufuatia mashambulizi hayo watu 15 waliuawa katika upekuzi wa makanisa Garissa katika mji ulio karibu na Somalia.

Mipaka ya Kenya imekuwa sio salama tangu ilipotuma askari wake kwenda Somalia kupambana na kikundi cha kiislam la Al Shabaab

Adan Wachu ambaye ni kiongozi wa Baraza Kuu la Kiislam nchini Kenya aliiambia BBC kuwa uvamizi huo ni kitendo cha kigaidi.

"Kuna watu pale wanaotaka kuifanya Kenya kuwa kama Nigeria nyingine,” alisema Wachu

No comments:

Post a Comment