TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 11 July 2012

Wastara kuzindua filamu ya SAYLA iliyolenga kumsaidia Sajuki

Kushoto ni Wema Sepetu, Wastara Juma na Angela Karashani ambaye ni muhusika mkuu katika filamu hiyo.

MSANII Wastara Juma akiwa na jopo la wasanii la  watu maarufu kutoka katika kada mbalimbali nchini wanatarajia kuzindua filamu yao mpya itakayokwenda kwa jina la Sayla.

Filamu hiyo imepangwa kuzinduliwa katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam. 

Aidha filamu hiyo itazinduliwa Mkoani Dodoma ambako inatarajiwa Wabunge wanaondelea na bunge la Bajeti nchini watahudhuria.

Wastara aliwataja  baadhi ya wasanii na watu mashuhuri waliocheza filamu hiyo kuwa ni pamoja na msanii nyota nchini wa kike Wema Sepetu, huku baadhi ya watu mashuhuri ni pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji.

Wabunge wengine ni Ester Bulaya (Viti Maalum CCM), Halima Mdee na Zitto Kabwe (CHADEMA), watangazaji maarufu ni pamoja na Maimatha Jesse, Ephraim Kibonde na wengineo wengi.

Katika filamu hiyo Wastara na yeye amecheza huku mhusika mkuu ni Angela Karashani , filamu hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Dynamic Minds.

Mwisho Wastara ambaye ni mke wa muigizaji  Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amewashkuru Watanzania kwa msaaada wao wa hali na mali na kuwataka wamuunge mkono katika  ununuzi wa wa filamu hiyo ambayo mapato yake yatakwenda katika kumsadia Sajuki na familia yake kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment