TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 6 August 2012

Vodacom yazindua mashindano mapya kwa watengenezaji program wa kujitegemea

 
Waendelezaji wa program za kiteknolojia wa Tanzania wanatarajia kunuifa baada ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom kuzindua  mashindano ya kutengeneza Programu ya kujitegemea ambapo mshindi atapata zawadi ya Sh Milioni 30.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni hiyo Kelvin Twissa inaeleza kuwa mashindano hayo yatakuwa katika awamu mbili, awamu ya kwanza hapa nchini na washindi kushiriki mashindano ya pili nchini Afrika Kusini.

Alisema  kuwa washiriki wataangalia mahitaji ya watanzania na kutengeneza Programu inayofaa ambayo itatumiwa na jamii kama zinavyotumika Google au mtandao wa kijamii wa Facebook ambayo itamnufaisha mtengenezaji na kubadilisha maisha yake itakapoanza kutumika.

Twissa alisema mashindano yameanzishwa ili kuwapa motisha vijana ambao wanaendeleza ubunifu wa kiteknolojia katika simu, hivyo shindano linatoa nafasi kwa washiriki kuonesha uwezo wao katika kuvumbua vifaa mbalimbali vinavyoweza kutumika katika nchi zinazoendelea na kutatua matatizo yanayoikumba jamii.

Alisema washindi watakaopatikana katika mashindano ya awali ndani ya nchi shiriki ambazo ni Tanzania, Misri, Lesotho, Afrika Kusini na Qatar watapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu na kuongeza Mshindi wa hapa nchini Vodacom itamdhamini kushiriki mashindano ya kimataifa.

Alisema katika mashindano ya ndani washiriki wanatakiwa kuendeleza ubunifu katika vipengele mbalimbali kama michezo, afya ya jamii, burudani na simu. Mshindi mmoja katika kipengele atapata dola 2000 za Marekani, na baada ya hapo kwa mshiriki ambaye atakuwa ametoa program bora atapata nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Twissa ni kwamba maombi yatawekwa na kusambazwa kupitia hifadhi ya program ya Vodacom na Vodafone na watu binafsi kuendelea kukusanya hadi mwisho wa muda wa kuwakilisha.
Alisema Vodacom kama muasisi wa mashindano hayo yaliyopewa jina la Appstar Challenge, inaalika washiriki kuzichapisha program zao kwenye hifadhi ya Vodacom au waende ofisi za Kinu ambapo mwisho wa shindano ni Septemba 3 mwaka huu.

Twissa alibainisha kuwa katika mashindano ya kimataifa, program mbili zitakazoshinda zitapelekwa katika mchujo wa wataalamu wa kimataifa kutoka Vodacom na washiriki wataonesha kazi zao mbele ya majaji hao kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment