TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 14 August 2012

Zanzibar Kuanzisha Mamlaka Kusimamia Mafuta yake

Na Rushyd Ahmed

SERIKALI ya Zanzibar inakusudia kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji. Waziri wa Maji, Ardhi, Makazi na Nishati, Ramadhani Abdallah Shaaban, ameliambia Baraza la Wawakilishi.

Waziri alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kin…achoendelea Chukwani, Zanzibar.

Alisema tayari mataarisho ya Sheria ya kuanzisha Chombo hicho yameanza, sambamba na Sheria za kusimamia na kusambaza nishati ya mafuta na Petrol ya Zanzibar.

“Mheshimiwa Spika kwa ajili ya kutekeleza sera ya Nishati Zanzibar, Wizara inaendelea kujiandaa pamoja na kuwapatia mafunzo wafanyakazi katika sekta ya nishati na mafuta,” alisema Waziri Shabaan.

Alisema juhudi za kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa Wizara hiyo zinalenga kukabiliana na upungufu wa wataalumu wa fani ya nishati ikiwemo kutafuta na kuchimba mafuta katika Visiwa vya Zanzibar.

Aidha, alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Serikali ya Norway inafanya mpango wa kufanya semina na kongamano kwa lengo la kutoa taaluma kuhusu athari za kimazingira zinazotokana na kutafuta na kuchimba mafuta Zanzibar.

Kuhusu tathmini ya kimazingira inayotokana na mwelekeo wa kutafuta na kuchimba Mafuta na Gesi asilia, Waziri alisema Wananchi katika Visiwa hivyo wamekuwa na matumaini makubwa ya kuwepo kwa nishati hizo.

Waziri Shabaan, alisema katika mwaka wa fedha unaoanza, Wizara yake pia imepanga malengo ya kuendelea na juhudi za kuwapatia wananchi wa Zanzibar elimu juu ya matumizi ya nishati.

SOURCE: Swahili Villa

No comments:

Post a Comment