TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 25 October 2012

Sheria za Tanzania ziboreshwe

Wakati Watanzania tuko kwenye maandalizi ya kutunga katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado mimi nasisitiza sheria za nchi ziboreshwe kwani limezuka wimbi la watu kutokuogopa wala kujali sheria. Mumejionea wenyewe mambo wanayofanya hawa binadamu.
Kuna baadhi ya matukio ya hivi karibuni yanathihirisha kuwa bado kuna haja ya kuwafanya binadamu waogope kutenda maovu. Adhabu kama za kifungo cha miaka 30 au kifungo cha maisha bado ni adhabu ndogo sana.
 
Mtu anayetaka eti kuingia Ikulu kwenda kumuona Rais wakati amebeba mawe au panga na yuko Waziri mwenye mamlaka hataki kwenda kumuona huyu kifungo chake ni Maisha na ikidhihirika dhana yake ni kumdhuru Rais tena wa Jamhuri huyu anyongwe hadi kufa.
 
Wanataka kutuingiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe hawa. Anyongwe hadi kufa. Rais ndiye anatakiwa kutangaza hali ya hatari wewe unatangaza kama nani wewe kikaragosi. Alafu unakimbilia Ikulu mwenyewe hata hayupo. Hawa ndio wabakaji, wezi, wachawi, wala unga, wavuta bangi, wanywa gongo. Sitaki kusikia habari zao wapewe adhabu kali sana. Manaenda Ikulu tumewapigia kura za ndio.
Kwa kuwa Rais ni mtu aliyepewa madaraka na Watanzania awe kwa kushinda kura au kwa kuchakachua lakini akishakuapishwa kuwa ni Rais hakuna tena mambo ya kusema kaiba kura.
 
 Huyu lazima tumpe heshima zake. Sasa wavuta bangi, wanywa gongo, na wabuya unga wanajikusanya tu na kudai wanataka kwenda Ikulu kumuona Rais mimi nadhani sio sawa. Hawa watu wanataka kuleta uvunjifu wa amani kwani Rais akipata matatizo nchi nayo inaingia kwenye matatizo bila kujali huyu ni CCM, CUF, CHADEMA, NCCR, SAU, au TLP. Hawa wakora waliotaka kwenda Ikulu wapewe adhabu kali sana kila mtu ajue kuna Serekali.
Mwisho vitendo vya watu kuchukua sheria mikononi na kuanza kuashibu wenzao kwa kuchoma makanisa na misikiti iliyojengwa kwa gharama mimi naona adhabu yake ni kifungo cha maisha au kunyogwa. Hatuwezi vumilia watu wanaleta tabia za udini udini ndani ya nchi wanaangaliwa tu kama vile hakuna sheria. Hii ni kunyima haki za watu wengine za kuabudu dini wanazotaka.
 
 Mtoto wa miaka 14 bado no mdogo sana kujua athari za kukojolea msaafu. Huyu adhabu yake ni bakora tu. Unachoma Kanisa kwa ajili ya motto kama huyu na hata historia yake hauijui. Hawa wote waliohusika adhabu yao kifungo cha maisha au kuntogwa labda tu wawe wana umri chini ya miaka 18 ndio sheria ziangalie adhabu inayowastahiki.
Kiongozi yeyote ndani ya nchi anayesababisha mikusanyiko ya dini au ya Siasa isiyo halali lazima sheria ichukue mkondo wake. Mimi nasisitiza hilo kwani kuna watu wanajifanya wanamjua Mungu kuliko wenzao. Kila mtu anajua Mungu yupo ni yuko hai na anaishi, na ataishi milele na milele. Lakini huwezi kuwashurutisha wenzako kuchoma Makanisa au Misikiti kwa visingizio, eti huyu kakojolea Msaafu, eti oh Yesu sio Mungu wewe inakuhusu nini kama Yesu sio Mungu.
 
Fuata Mchungaji wako au Shehe wako anakufunza nini katika imani yako ya Dini. Majigambo, Masifa na mabishano barabarani sio kuwa mcha Mungu. Umesikia watu wanabishania Dini wewe kimbilia Biblia yako au Msaafu wako soma kila mstari unaozungumzia hayo mabishano utapata jibu.
Mwisho namuomba mheshimiwa Rais akubali kuweka saini kwenye karatasi anazoletwewa na Majaji zenye adhabu ya kifo. Watu tumekuwa wakaidi. Bila adhabu kali kuwepo kwenye katiba ya Jamhuri utawakuta watu wako Ikulu wanataka nao wale na Mheshimiwa au walale Kitanda cha mheshimiwa huu ni ukora lazima tuukomeshe. Wanyongwe hadi kufa.
 
Mkereketwa
Lengai Ole Letipipi.

No comments:

Post a Comment