Tanzania tumebahatika kuwa na
rasilimali za kila aina ikiwepo madini, wanyama, ndege, bahari, maziwa, malima,
ardhi, misitu na kadhalika lakini Mwenyezi Mungu akatunyima viongozi bora.
Toka
afariki Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tumekuwa yatima kama Watoto
wa vifaranga ambavyo Mama yao
amechukuliwa na mwewe. Watanzania hatuna haki katika nchi yetu. Viwanda wameua,
Viwanja vya wazi wamegawana, Mashamba ya Serekali wamegawana. Nchi imekuwa
mufilisi. Mimi hata sioni sababu ya kuzungusha Mwenge wa Uhuru. Hiyo fedha
wapeni watoto yatima na wajane mtapata fadhila.
Viongozi
wanasimama majukwaani kutangaza sera nzuri sana
mbele ya watu waliowapigia kura lakini wakishafika maofisini ni kama wamelogwa. Hebu shuhudieni haya hapa chini.
-Kiongozi
anakaribisha Wawekezaji kwenye sekta ya madini lakini nchi inaambulia asilimia
tatu tu ya madini yanayochibwa nchini.
Serekali
imekuwa sio sikivu tena Viongozi wamekuwa wafanya biashara. Watu wanafanya
biashara Ikulu. Nani asiyejua kuwa Ikulu imekuwa ya biashara. Nani asiyejua
kuwa karibuni miradi yote ya wawekezaji nchini wako viongozi wakubwa ndani.
Nani asiyejua kuwa viongozi wetu waliviua viwanda vya ndani ili wafanye
biashara.
Kama sivyo kulikuwa na haja gani
kukiua kiwanda cha Matairi kule Arusha na kila siku Watanzania wananunua
magari. Mimi nasema lazima tujaribu watu wengine CCM sasa basi. Wameweka watoto
wao madarakani ili kuitawala Tanzania
kama Koloni lao. Aliyeishitaki Serekali ya CCM
kwenye mahakama ya Kimataifa alifanya vizuri sana
na nampa heko.
Wakitaka ushahidi walete waonyeshe mashule wanayosoma watoto masikini,
waomyeshe zahanati zetu, waonyeshe viwanda walivyoua, waonyeshe makaburi ya
Alibino na makaburi ya watu waliouwawa na Polisi. Wakitaka ushahidi zaidi tupo
Watanzania ambao tutatoa ushahidi mpaka wa Mali zao wanazomoliki.
-Kiongozi
anapita kuwaomba Watanzania kura za ndio lakini akishazipata anatuma watu
kuwavunjia watu hao hao makazi yao.
Kinachofanyika
sasa hivi Tanzania
ni ukora na uonevu kwa watu wanyonge. Mimi naishangaa Serekali sikivu kwa
kuomba kura za ndio lakini watu wanapovunjiwa nyumba zao na kulala na familia
nje haiwakeri. Nawashangaa Watanzania kuikumbatia Serekali sikivu saaa ya
uchaguzi lakini uchaguzi ukipita wanalia na kusaga meno. Maisha imekuwa magumu sana kiasi kwamba mtu
anayepata mlo mmoja kwa siku anashukuru Mungu. Wengi wa Watanzania sasa hivi
hawali wanashinda njaa kutokana na ukame lakini Serekali sikivu ipo. Serekali
sikivu wananchi wanalala nje. Serekali sikivu watu wake wanapigwa risasi hovyo.
Ameuwawa Mwangosi hamkutoka maofisini. Ameuwawa Askari tena labda kwa bahati
mbaya au labda kwa kugombania wanawake watu wote wametoka maofisini. Kamanda
wetu kauwawa kwa bahati mbaya tu, mbona Mwangosi aliuwawa kwa makusudi lakini
hata tume mliyounda wenyewe imepindisha maelezo. Tunaomba watu zaidi wajitokeze
kuishitaki Serekali ya CCM kwenye mahakama ya Kimataifa. Wanazo kesi za kujibu.
Kama hawana kesi za kujibu kwa nini Waziri
mkuu alilia ndani ya Bunge.
-Kiongozi
anatumia mabilioni kutangaza utalii ili watu waje kwa wingi wakati huo huo anaongeza
bei za kuingia kwenye hifadhi wakati huo huo anafanya biashara ya kuuza wanyama
na ndege.
Mimi
huwa naishangaa Tanzania sio
bure Kadfa wa CCM ndugu Kusila akasema Tanzania inapelekwa Mochwari. Hivi
kama unauza Wanyama na ndege nje ya nchi maana yake si hao watu wanaenda fungua
hifadhi zao za ndani. Sidhani kuwa wanaenda kuwala. Kama wanaenda fungua Zoo za
kuweka wanyama maana yake si kwamba wanapunguza idadi ya Watalii kuja Tanzania.
Tunaona ugumu gani kuwachinjia watoto wa shule nyumbu wakala kuongeza
virutubisho mwilini kuliko kuwauzia Watu wakafungua Hifidhi zao za wanyama
ndani. Ukimuuza mnyama na ndege wako huku unapandisha bei za kutembelea hifadhi
matarajio yako ni nini hasa. Watu wanachimba madini ndani ya hifadhi za Taifa
kule Serengeti mpaka Watanzania wananyimwa kupita na watalii maeneo hayo. Watu
wanaporwa aedhi yao
kwa ajili ya wawekezaji. Mimi napenda tu hata hao wanaosaidiwa kupora wajue Tanzania ni ya
Watanzania na sio ya mtu wa kuja. Kama
waliweza Wazimbabwe kuwatoa wawekezaji sisi Watanzania tutashindwaje?. Kilichonishangaza
zaidi ni kuingilia hata ardhi yetu Masaini kule Ngorongoro. Jiandaeni sana lakini niwajulishe
tu kuwa La Mgambo limelia na likilia kuna jambo!
Mkereketwa!
Lengai
Ole Letipipi
No comments:
Post a Comment