Mimi sidhani maisha bora yanaletwa na
kujenga barabara na wala sidhani kutembea sana Duniani ndio maendeleo. Kagame,
Mwai Kibaki, Museven, Mugabe wameenda mara ya mwisho Ulaya lini mbona wanayo
maendeleo. Wala Tanzania mbele ya Wakenya, na Wanyarwanda tusiongee kitu kabisa.
Sisi tutaendelea kudangaywa na Siasa mpaka mwaka 2015 tutwapigia tena
kura. Maendeleo ya Barabara huku watu wako hawajui kusoma na kuandika ni
maendeleo gani?. Maendeleo ya Barabara huku watu wako hawana ajira ni maendeleo
gani?. Kwani Barabara zikiwa za vumbi lakini Watoto wanaomaliza shule wanakuta
viwanda kede kede na kupata ajira kuna shida gani?. Barabara Tanzania safi
lakini afya za watumiaji matatani, hoi bin taabani. Elimu ndio usiseme.
Kama ni mimi Rais Jakaya Mrisho namfukuza kazi Magufuli kwa
kunikejeli. Yani Watanzania wote wanalalama kuwa Safari za mheshimiwa zimezidi
na zinatia hasara yeye anasema zinaleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Tumefaidika nini na safari zake wakati nchi inadaiwa trilioni 22. Miaka 50 ya
Uhuru wa Tanganyika watoto wanakaa chini wakiandika, Hakuna Zahati wala Madawa
ya Tiba, Wanafunzi wanamaliza shule hakuna ajira viwanda vyote kwishnei, alafu
mnasema kusafiri ndio maendeleo.
Watanzania wanakaa nyumba za tembe nyie
mnajenga mabarabara mpitishe malori yenu kwendeni zenu huko. Kwani hatujui
Ridhiwani ndiye anajengewa barabara malori yake ya mafuta yasimwingize gharama
za kununua spea. Nani mjinga Tanzania hii siku hizi.
Au maendeleo ni
kuficha fedha Ulaya, au Kuuza meno ya Tembo, au kuuza Wanyama, na kufanya
biashara ya kuuza watu kama sasa zinavyofanyika. Au Watanzania hamjui Tanzania
kuna biashara ya utumwa. Kule Arusha kuna Tajiri anaitwa Salum Ally yuko rumande
kisa amewarusha wakubwa kwenye biashara ya kuuza watu.
Wamefanya naye Biashara
ilivyofika uchaguzi alivyokataa kumchangia Matylda wakamsweka ndani yuko Segerea
ananyea kwenye ndoo. Tanzania bwana mambo ya ukandamizaji siku hizi wazi wazi.
Mnataka kuniambia Barabara na Elimu na Afya za Watanzania kipi bora. Hii miradi
wanaojisifu nayoni kodi za Watanzania wamelipa na ukikaa kufanya mahesabu
bado wameiba sana. Alimasi, Dhahabu, Tanzanite, Gasi, Makaa ya Mawe, Wanyama,
Milima kweli tunadanganyiwa visima vya maji.
Mimi nashukuru Serekali imejenga barabara
lakini kwa ujinga wangu nilionao sidhani hizi barabara zina faida yoyote kwa
Watanzania kama fedha hizo zingetumika kufufua viwanda, Mashirika ya Umma,
Mashule safi, Hosipitali safi, nk. Barabara mimi ningeshauri zisipewe kipaumbele
kuliko Afya za watu na Elimu. Watanzania wangapi wanaouwezo wa kusafiri kwa
kutumia hizo barabara. Watanzania wangapi wanazo hata baiskeli za kutumia hizo
kilometa za barabara. Nchi imejaa Migomo kila mahali, Walimu, Madaktari,
Magereza, nk.
Watu wanadai Mishahara na marupurupu yao. Fedha nyingi sana za
Watanzania zinatumika vibaya hasa kwenye kura. CCM inatumia mda mwingi sana
kwenye kuchaguana. Angali ni mavazi aina ngapi wanavaa kwenye mikutano yao na
chaguzi zao. Angalia fedha zinazotumika kwenye vipeperushi vyao. Watanzania
lazima tubadilike. Watanzania tumetelekezwa na Serekali kwa kununua kila huduma.
Kuanzia Elimu, na Afya. Bidhaa madukani hazishikiki mnasema maisha bora.
Ukilinganisha rasilimali tulizo nazo na huduma zitolewazo na Serekali ya CCM ni
udanganyifu mtupu. Lazima mabadiliko!
Mkereketwa
Lengai Ole
Letipipi
|
Tuesday 6 November 2012
Asemavyo mkereketwa kuhusu ujenzi wa barabara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment