TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 19 April 2013

Ally Nipishe kuachia ngoma mpya siku za karibuniAlly Nipishe akifanya vitu vyake

MSANII mkali wa Jumba la Sanaa Tanzania (THT) Ally Nipishe amesema baada ya ngoma yake ya Mai kuendelea kufanya vizuri, anajiandaa kuja na ngoma nyingine mpya kabla mwezi huu haujaisha.

Akizungumza na safu hii, Ally Nipishe amesema anashukuru Mungu kwamba  wimbo wa Mai umekubalika, ambapo amekuwa akipata shoo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam na bado watu wa mikoani wamekuwa wakimtafuta kwa ajili ya shoo.

“Nashukuru Mungu kwamba toka nimetoa wimbo wangu wa Mai unaendelea kufanya vizuri, umekubalika kwa haraka kwasababu nimetoa ujumbe ambao ni wa kuelimisha jamii, napata shoo pia,”alisema.

Ally Nipishe amesema baada ya kuachia wimbo mwingine ambao hakupenda kuutambulisha kwa haraka, anatarajia kufanya kazi na wasanii nyota akiwemo Ally Kiba na Young Killer kwa vile ndio wasanii wanaomvutia kwa sasa.

  Msanii huyo kipaji chake kilianza kuvuma pale aliposhirikishwa na msanii wa kike anayetamba na ngoma yake kali ya Ni wewe, Mwasiti Almas, ambapo alionekana kufanya vizuri na ndipo mashabiki kumtaka kuja na wimbo wake ambao ndio unaovuma kona mbalimbali za redio nchini unaojulikana kama Mai.

No comments:

Post a Comment