Ussu Mallya |
MTANDAO wa
Jinsia Tanzania (TGNP) unatarajia kuzindua ilani ya madai ya wanawake kwenye
Katiba mpya Mei 8, mwaka huu katika viwanja vya
Ofisi zake zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Ussu
Mallya alisema TGNP kwa kushirikiana na wanaharakati wa masuala ya ukombozi wa
wanawake, usawa wa kijinsia, haki za Binadamu, utawala bora na Maendeleo
wamekuwa na utaratibu wa kuandaa ilani mbalimbali za wananchi kuanzia uchaguzi
wa mwaka 2000, 2005 na 2010.
“Mwaka huu
tumeandaa Ilani ya madai ya wanawake wa Tanzania kwenye katiba mpya, ili
kuwezesha jamii kuchambua, kujadili na kuangalia maeneo muhimu ya kudai
uwajibikaji na utekelezaji wakati wa mijadala ya kuandaa katiba mpya.
Alisema mchakato
wa kuandaa madai ya katiba mpya umetokana na ushiriki mkubwa wa wadau
mbalimbali yakiwemo mashirika katika ngazi ya kitaifa na jamii yanayotetea haki
za Binadamu, jinsia na maendeleo, Femact na GDSS ambazo hufanyika kila Jumatano
mabibo.
Kwa mujibu
wa Mallya alisema madai hayo yametokana na ushiriki na sauti mbalimbali za
wadau wanaotetea haki za wanawake na hususani haki zao za kikatiba na kuongeza
kuwa ni matumaini yao kuwa tume ya mabadiliko ya katiba inatambua changamoto
zinazowakabili wanawake ili yaweze kuingizwa katika katiba mpya.
No comments:
Post a Comment