TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 11 June 2013

Mnafu Enterprises kuipiga ‘tafu’ Taswa FC

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mnafu Enterprises imeahidi kutoa zawadi ya seti moja kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa FC) kwa ajili ya matumizi katika michezo yake mbali mbali
Mkurugenzi Mkuu wa Mnafu Enterprises, Mnafu Mmary alitoa ahadi hiyo juzi mara baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu Taswa FC na  Salasala Vision Group (SVG) Veterans iliyofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club.
Mmary ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa timu hiyo ya Salasala alisema kuwa amevutiwa na timu hiyo ya Taswa FC kwani wamedhihirisha kuwa wanaandika kitu ambacho wanakijua.
“Nimefurahi jinsi mlivyocheza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, nimehamasika sana kwa mchezo wenu na ninaamini kuwa mtaendelea kufanya vyema,” alisema Mmary.
Alisema kuwa atakabidhi jezi hizo kabla ya mechi yao ya marudiano iliyopangwa kufanyika Juni 22 kwenye uwanja wao wa Salasala.
Katika mchezo huo wa kuanzisha ushirikiano, Taswa FC iliibuka kwa mabao 3-2 yaliyofungwa na Majuto “Ronaldo” Omary alyefungwa mawili yote kwa njia ya mipira ya faulo ndogo nje ya eneo la hatari na Dennis Bukoli kwa njia ya penati. Mabao ya SVG yalifungwa na Paul Muache kufuatia pasi safi ya Peter Marwa na Yahya Mbanka baada ya kazi nzuri ya Charles Mtangi.

No comments:

Post a Comment