TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 9 September 2013

Filamu ya Foolsh Age kuonyeshwa kwenye tamasha la filamu la 'Dar Filamu Festival'

Lulu wa kwanza (kushoto)Mratibu wa DFF (katikati) Staford Kihore na kulia ni Godfrey Katula ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Haak Neel Production



FILAMU mpya ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu inatarajiwa kuonyeshwa kwenye tamasha la filamu linalofahamika kama ‘Dar Filamu festival’ (DFF) litakalofanyika Septemba 24 hadi 26 jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa tamasha la DFF 2013 Staford Kihore amewaeleza waandishi wa habari jana kuwa, tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu.



Alisema kupitia tamasha hilo, filamu hiyo na nyingine za kibongo ambazo zinatambuliwa na Bodi ya filamu Tanzania zitaonyeshwa bure kwenye viwanja vya Posta.


Alsiema tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania, na zile zinazotumia lugha ya kiswahli pekee ili kutoa fursa kwa ajili ya vijana na jamii husika kwa ujumla.


“Filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa hapa nchini katika kutangaza lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya filamu central kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu ulimwenguni,”alisema.


Sanjari na uonyeshaji wa filamu hizo, pia kutakuwa na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya sanaa ambapo watafundisha masomo ya uandishi wa muswada, uigizaji na uongozaji wa filamu ambapo makampuni ya utengenezaji filamu yatatumia fursa hizo kutangaza kazi zao.


Alisema siku ya mwisho kutakuwa na jukwaa la majadiliano kwa wadau wakiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), wadau wa bodi ya filamu na makampuni mbalimbali.


Naye msanii wa filamu za kibongo Elizabeth Michael amehimiza watu kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kuwaunga mkono.


Alisema ni muhimu watanzania wakajenga mazoea kupenda filamu zinazotengezwa nyumbani, hivyo kufika kwao kwenye tamasha hilo, kutawezesha kuinua kazi zao.

No comments:

Post a Comment