TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 24 September 2013

Push Mobile kutoa gari kwa mpenzi wa Fiesta

Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney
 
Mwandishi Wetu
Kampuni ya Push Mobile Media itatoa zawadi ya gari aina ya vits kwa mshindi wa promosheni ya tamasha la Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza ijumaa hii.
 
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa watatoa gari aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika tamasha hilo kwa kutuma neon Fiesta kwenda namba 15678 na kuigingia katika bahati nasibu hiyo.
 
Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda fedha taslimu kiasi cha shs 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta anaweza kushinda pikipiki.
 
Mshindi wa mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza wa gari alikuwa Abdallah Ally Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha la fiesta la Kigoma.
 
 “Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa  nguvu zote,” alisema Rodney.
 
Wakati huo huo; mkazi wa Shinyanga Rose Mahenda amafanikiwa kushinda pikipiki baada ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo.

No comments:

Post a Comment