TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 21 October 2013

Kilio cha wafanyakazi wa Shule kwa NSSF Mbeya

Wafanyakazi wa shule ya msingi St.Benedict na Sekondari ya Symbiosis mkoanai Njombe kata ya Ramadhani tulijiunga na mfuko wa jamii NSSF.

Kila mwezi tunakatwa pesa kutoka kwenye mishahara yetu. Chakushangaza na ndicho ambacho tunakilalamikia hii leo, ni kwamba mbali na kwamba tunakatwa lakini pesa zetu hizo hazipelekwi kwenye mfuko huo wa jamii.


Chakushangaza zaidi ni kwamba wengi wetu kadi za NSSF tunazo tena hizi za kisasa lakini hatuna pesa kwenye akaunti zetu. Tunajiuliza hivi utakuwaje mwanachama bila pesa kwenye akaunti na kadi unayo? 


Kwani hapa nani wakulaumiwa, ni huyu mwajiri wetu huyu mama wanaemwita mzungu mwenye shule hizo mbili au ni uzembe wa NSSF Njombe ambao tunavyojua  wamepewa meno na serikali ili kuwachukulia hatua za kisheria waajiri wote wanaofanya upumbavu kama huu wakukata pesa kwenye mishahara ya wafanyakazi wao na hawapeleki kunakohusika?


Huyu mama ambaye huwa huwalipa wafanyakazi wake mala tatu kwa mwaka (yaani miezi minne minne) bila kujari sheria za nchi, ukimwendea kumuliza kuhusu hili suala huwa mkali kama mbogo na unaweza hata
kufukuzwa kazi na usilipwe mafao yako. 


Kuna kipindi NSSF walifika shuleni hapo kumuona huyu mama mwaka huu wa 2013 lakini waliambulia kupewa cheki ambao haikuwa na hela benki. Mbali na kufanyiwa hivyo shirika hili la NSSF mkoani Njombe limekaa kimya kabisa bila kuchukua hatua zozote zinazostahili kana kwamba wanamuogopa huyu mama au hawalioni hili kosa kabisa.

 NSSF Njombe sisi tunauliza huyu mama amewashinda nini? Na hawa wafanyakazi wote hawa ambao kwa idadi ya haraka wanaokatwa NSSF hufikia zaidi ya 60, wakija acha kazi watakuwa wageni wa nani na watapateje hiyo pesa ama jasho lao wakati mwajiri wao hajawalipeni ninyi?

Tunaomba sana tena sana NSSF Njomba fuatilieni hizo pesa zetu kwa huyu mama lazivyo mtalaumiwa ninyi wenyewe kwakutudhurumu haki yetu na jasho letu. Tunafanya kazi kwakuteseka sana na kwenye mazingira magumu mno kwa huyu mama wa kizungu lakini bado pesa zetu za NSSF hatunazo wakati kila mwezi tunakatwa. Rais Kikwete tunaomba sana utuondolee dhuluma kama hii hapa. Huu ni udhulumaji wa wazi kabisa. 


Pesa zetu tukatwe harafu zisionekani, zinaenda wapi? Chonde chonde vyombo vyote vinavyohusika na kutetea wafanyakazi hasa ambao wanadhurumika kama sisi tusaidieni kutetea haki yetu hii. Tupelekewe pesa zetu kwenye akaunti zetu NSSF. 

Uongozi wa NSSF taifa hebu angazieni macho huku NSSF Njombe, wanafanya nini? Je, wanachukua kitu kidogo kwa huyu mzungu? Hebu chunguza hili suala huenda kuna mkono wa mtu hapa maana
sasa tunakosa imani na shirika hili. Kwa mawasiliano zaidi andikeni kwenye barua pepe hii
ejohn179@gmail.com.

No comments:

Post a Comment