TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 30 October 2013

Timu ya kuogelea yashinda medali 72TIMU ya Tanzania ya kuogelea ‘Swim Squad’  imefanikiwa kutwaa  medali 72 ilizoshinda kwenye mashindano ya kuogelea ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika bwawa la Oshwal academy Mombasa Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Kuogelea Tanzania(TSA) Ramadhan Namkoveka, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha nchi tatu za  Uganda, Tanzania na Kenya, Tanzania iliwakilishwa na wachezaji 42 na tayari  ilirudi juzi  usiku na ushindi huo wa kuridhisha.


Alisema kati ya medali hizo, 22 ni  medali za dhahabu  25 za fedha  na  25 za shaba. Kutokana na mashindano hayo timu hiyo ya Tanzania imeshika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia alama 282 kati ya timu 27 zilizoshiriki.

Mshindi wa kwanza kwa wanawake ni timu ya Braeburn ya Kenya iliyopata alama 466, ikifuatiwa na Seahorses ya Kenya pia  iliyopata alama 282.

Namkoveka alisema kwa wanaume timu ya Tanzania Swim Squad imeshika nafasi ya pili na kukabidhiwa kikombe  baada ya kupata alama 271 ambapo mshindi wa kwanza ni Braeburn iliyopata alama 410 na timu ya bandari ya Mombasa imepata alama 212.

Mchezaji bora kwa upande wa wanawake miaka 12-13 ni Kimberly Hind wa Braeburn alama 24, Imara Thorpe kutoka Shule ya Banda School  mwenye alama  23 na Sonia Tumiotto wa Tanzania Swim Squad kashika nafasi ya 3 kwa kupata alama 17.  Washindi wote hawa wamepata vikombe.

Mchezaji bora wanawake miaka 10-11 ambao pia wamepata vikombe ni Hadasa Mumbi Gichovi wa Loreto , Kenya , alitepata alama 37. W apili ni Gloria Muzito wa Dolphins ya Uganda aliyepata alama 27 na wa tatu ni Emma Imholf wa Tanzania Swim Squad aliyepata alama 17.

Mtanzania Catherine Mason mwenye umri wa miaka 16 anayesoma Mombasa wa timu ya Bandari ya Mombasa amekuwa mshindi wa kwanza kwa wanawake kwa kupata alama 28, akifuatiwa na Natasha Owino wa Seahorses ya Kenya aliyepata alama 25, na Akinyi Ogot wa Baracuda aquatic ya Kenya amepata alama 20.

Kwa upande wa wanaume mchezaji bora ni Tory Pragasa kutoka Bandari ya Mombasa amepata alama 45, wa pili ni Hilal Hilal kutoka Tanzania kwa kupata alama 34 na Edward Ilako wa Seahorses ya Kenya alikuwa wa tatu kwa kupata alama 17.

No comments:

Post a Comment