TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 21 November 2013

Miss Universe arejea nchini kutoka Urusi


Na Mwandishi Wetu

Miss Universe Tanzania, Betty Boniface Omara amerejea nchini kutoka Urusi alipokwenda kushiriki katika mashindano ya kimataifa na kukiri kuwa mashindano hayo ni magumu pamoja na kupata uzoefu mkubwa.Betty ambaye aling’ara katika vazi la Taifa kwa kuvaa vazi lilobuniwa na mbunifu chipukizi, Mwanakombo Salim kwa kusaidiana na wasanii wa Tingatinga, alisema kuwa pamoja na kutofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, anachojivunia ni kuweza kuitangaza nchi kwa kupitia vivutio vya utalii akiw balozi wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) ambao walikuwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Universe Tanzania.

Alisema kuwa mbali ya hayo, alikuwa mrembo pekee kutoka bara la Afrika aliyechaguliwa miongoni mwa warembo nane kote ulimwenguni kushiriki katika kipindi maarufu mjini Moscow kinachoonyeshwa duniani kote kijulikanacho kama “Let Them Talk” kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu Andrey Malakhov.Betty alisema kuwa katika kipindi hicho ambacho kinapatikana kwenye mtandao, alionekana kuwafurahisha sana hadhara ya warusi katika studio na kusifiwa kwa kuwa mrembo wa kipekee na mwonekano wake wa kiafrika.Alifafanua kuwa baadhi ya majaji wa mashindano ya Miss Universe walikuwepo na walieleza kuvutiwa sana na Betty na kumwona kama mrembo ambaye alikuwa ana nafasi kubwa ya kuingia 16 bora.Kipindi chote nilipokuwa Urusi, niliona kukubalika sana na warusi wenyewe na hata vyombo vya habari vya kimataifa. Nina furaha kubwa sana kwani kilichonileta nimekifanikisha kwani lengo langu kubwa zaidi ya ushindi ilikuwa ni kuhakikisha naitangaza vyema Tanzania na vivutio vyake, kama vile hifadhi za taifa za Ruaha, Udzungwa, Katavi na mengineyo” alisema Betty.Alisema kuwa kwa msaada mkubwa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, alifanikiwa kufanya mahojiano na gazeti maarufu la utalii nchini humo lijulikanalo jarida la utalii nchini Urusu linaliitwa “Hot Line travel Magazine.”Betty alivalishwa na Mama Schwari, Kiki Zimba (Kiki’s), Kali Elegance na Nasreen Kareem kupitia duka lake la Anjipai ambapo alimpa nakshi ikiwemo mikufu na hereni  mbalimbali katika kukamilishia mavazi yake na kuonekana kiafrika zaidi.

No comments:

Post a Comment