TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 6 November 2013

Miss Universe atamba Moscow

Miss Universe Tanzania, Betty Boniface Omara ametamba katika maonyesho ya mavazi kwa warembo 85 wanaowania taji la Miss Universe la mwaka huu mjini Moscow.
 
Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Vegas Mall, vazi la Betty lililobuniwa na mbunifu anayekuja kwa kasi nchini, Mwanakombo Salim, lilipendwa na mashabiki wengi na anamatarajio makubwa kushinda taji hilo wakati wa fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Jumamosi.
 
Vazi hilo limechorwa na wasanii wa Tingatinga, Said Kambili na Mimus, michoro ambayo ni maarufu nchini iliyoasisiwa na msanii maarufu wa zamani, hayati Edward Tingatinga. Vazi hilo hilo mbali ya kudumisha utamaduni wa Tanzania, pia limechorwa michoro mbali mbali ya kuvitangaza vivutio vya kitalii.
 
Vazi hilo pia lina nakshi za mkeka na miba ya  mnyama maarufu ajulikanaye kwa jina la Nungunungu. Vilevile pia umetumika kama njia ya kumuonyesha ndege Tausi kama inavyoonekana rangi za mkeka kwenye mkia na kilemba kichwani mwake.
 
Lengo kuu la nguo na michoro hii ni kutangaza kazi za mikono na  utalii wa Tanzania na miongoni mwa michoro iliyoonyeshwa ni Duma, Tembo na Twiga vilevile imeonyesha ndege na mali asili zipatikanazo Tanzania kama vile Tausi, vipepeo, mimea na Mlima Kilimanjaro.
 
Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa.  

No comments:

Post a Comment