TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday, 15 December 2013

Dunia yamuaga Tata Mandela

 Na Bbc Swahili

Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela amezikwa katika kijiji cha Qunu mkoa wa Cape Mashariki nchini Afrika Kusini.

 

Mjane wa Mandela Graca Machel pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma walikuwepo katika hafla ya mazishi iliyohudhuriwa na jamaa za karibu wa familia ya Mandela pamoja na viongozi wengine wakuu.

Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa walihudhuria mazishi hayo ambayo yalikuwa ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.

Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi hayo.

Kiongozi mmoja wa kitaduni aliita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.

Viongozi wa Afrika, familia na marafiki walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.

Rais Jacob Zuma alisema kuwa safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha lakini raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.

Mandela alifariki tarehe 5 mwezi Disemba akiwa na umri wa miaka 95.
Siku ya kumi na ya mwisho ya maombolezi kufuatia kifo cha Mandela, imekamilishwa na Mandela kupigiwa mizinga 19 na jeshi huku mwili wake ukizikwa katika kijiji cha Qunu. Mishumaa 95 iliwashwa kila mmoja ikiwa ishara ya miaka ya Mndela

No comments:

Post a Comment