TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 5 December 2013

Mfalme wa Thailand ahimiza mshikamano


 Mfalme Bhumibol Adulyadej wa Thailand amewataka wananchi wa nchi hiyo kushikamana kwa manufaa ya nchi hiyo, katika hotuba yake kwa taifa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Thailand inaadhimisha miaka 86 ya Mfalme huku kukiwa na mkataba wa kusitisha ghasia baada ya siku kadhaa za maandamano mjini Bangkok, Thailand.

Akizungumza katika makao yake yaliyopo Hua Hin, mfalme alisema kuwa Thailand imekuwa na amani kwa sababu ya umoja wa watu wake.

Mapema wiki hii kulikuwa na mapigano makali kati ya polisi na waandamanaji.

Waandamanaji ambao wamekuwa wakitaka serikali ijiuzulu, walianza kuandamana tarehe 24 Novemba mwaka huu.

Walikubali kuacha kushambulia majengo ya serikali ili kupisha sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa mfalme wa nchi hiyo, lakini wakisema wataendelea na maandamano yao baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.

Wananchi wa Thailand ambao wanamheshimu sana Mfalme King Bhumibol Adulyadej, ambaye kwa sasa anaishi katika eneo la Hua Hin. 


Watu walijitokeza katika mitaa kumtakia heri mfalme wakati huu wa ghasia nchini humo.

Alhamisi, maelfu ya watu walielekea katika mji wa Hua Hin, karibu na makaazi ya mfalme ya Klai Kangwon, kwa matumaini ya kumwona.

Source:Bbc Swahili

No comments:

Post a Comment