TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 18 June 2014

Ghana yakana mgawanyiko kikosini Na Bbc Swahili
Ghana ilicharazwa na Marekani mabao mawili kwa moja dhidi ya Marekani katika mechi yao ya kwanza.


Shirikisho la soka nchini Ghana, limekanusha ripoti za kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba timu ya taifa ambayo inashiriki michuano ya kombe la dunia imekumbwa na mgawanyiko hasa baada ya kushindwa na Marekani mabao mawili kwa moja Jumatatu.

Kulingana na kituo hicho cha Joy FM, huenda wachezaji wamegawanyika na kumkataa kocha mkuu, hali ambayo ililazimisha maafisa wa timu hiyo kufutilia mbali mkutano waliokuwa wameandaa na waandishi wa habari Jumanne.

Shirikisho hilo limesema: ''Tunataka kuthibitisha kuwa ripoti hizo sio za kweli na hazina ushahidi wowote.''

"hakuna mchezaji hata mmoja ametofautiana na kocha Kwesi Appiah."

Wachezaji wanajiandaa klwa mechi nyingine Alhamisi ijayo
 
Taarifa hiyo iliongeza kusema, "hakuna mchezaji au wachezaji wamehusika na njama ya kukataa kucheza pamoja na kumpinga kocha mkuu. ''

"mkutano ambao tulikuwa tumeandaa na wandishi wa habari ambao ulipangwa kufanyika saa tano saa za Brazil, ulikuwa wa wasimamizi wa timu wala sio wachezaji. 

Ulibadilishiwa muda na kupangwa kufanyika saa kumi na nusu jioni kwa sababu kikosi kilikuwa kimeswali kuchelewa.''

Wachezaji wote 23 wa timu ya taifa ya Black Stars, walikuwepo tayari kwa mkutano kwa mwongozo wa Appiah.

Tunataka kuwahakikishia wananchi wa Ghana kuwa kocha Kwesi Appiah na wachezaji wake, wanaangazia zaidi mechi yao dhidi ya Ujerumani wiki ijayo, na wako makini kushinda mechi hiyo.

Baada ya mechi ya Ujerumani, mechi ya mwisho ya Ghana itakuwa dhidi ya Portugal Alhamisi wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment