TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday 5 October 2014

Rais Kikwete atoa Ng'ombe kwa wananchi wa Monduli

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009. Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Makuyuni,wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Rais Kikwete akielekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli.

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Makuyuni,wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Rais Kikwete akiwa na viongozi wenzie kwenye meza kuu.

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,wilayani Monduli mchana wa leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza kuwakumbuka wananchi wa wilaya ya Monduli.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng'ombe kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.(chanzo swahiliblog)  

No comments:

Post a Comment