TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 29 September 2015

Taarifa ya Mbeya City kuhusu Nyoso

DSC_0060
Bodi ya klabu ya Mbeya City ilikutana jana tarehe 29.09.2015 kwa dharura kulijadili suala ambalo hivi sasa linaendelea kujadiliwa katika Umma wa wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa timu yetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam Fc uliochezwa tarehe 27.9.2015 katika uwanja wa chamanzi.

Katika kikao hicho kilichomalizika hivi punde,yafuatayo yameamuliwa
Kwa kuwa katibu Mkuu wa Klabu jana aliiagiza idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Klabu kulifanyia utafiti suala hili,Bodi imeiongezea idara hiyo wajumbe wawili ili kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa adidu za rejea zifuatazo:

(a) Kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia Mazingira na Asili ya suala zima lililojitokeza.


(b) Kupata Maelezo ya awali ya mchezaji wetu juu ya suala lenyewe.
(c) Kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha watalaam wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha kuishauri Bodi.


2. Kazi hii iwe imekamilika ndani ya masaa 86 kuanzia jana saa saba mchana ilipoanza.


Klabu inaomba umma wa wan
umma wa wanamichezo kuwa na subira.
Kazi hii iwe imekamilika ndani ya masaa 86 kuanzia jana saa saba mchana ilipoanza.

Klabu inaomba umma wa wanamichezo kuwa na subira.
Wasalaam,
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC

No comments:

Post a Comment