TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 6 October 2015

Tuzo za Taswa Oktoba 12

 Sherehe za utoaji tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwa miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete sasa zitafanyika Oktoba 12 badala ya tarehe iliyotangazwa awali.
 
Taswa licha ya kutoa tuzo kwa wachezaji waliofanya vizuri zaidi, pia itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni  kuthamini mchango wake katika michezo wakati wa uongozi wake.
 
Baadhi ya mambo hayo ni serikali yake ilivyolipia  makocha wa michezo ya soka, netiboli na ngumi na pia serikali ilipeleka wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya kimataifa. 
 
Pia serikali yake ilirejesha michezo shuleni pamoja na mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari (UMITASHUMTA na UMISETA).
 
Pia tukio hilo la tuzo itakuwa sehemu ya wanamichezo kumuaga Rais Kikwete ambaye anamaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 
Maandalizi muhimu kwa tukio hilo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kupata majina ya wanamichezo hao watakaopewa tuzo siku hiyo.
 
Alhamisi wiki hii Taswa itatangaza wadhamini wengine watakaoungana na wadhamini ambao tayari wametangazwa ambao ni GSM Foundation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
 
Ahsnateni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
05/10/201

No comments:

Post a Comment