TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 30 November 2015

Kili Stars yatolewa Chalenji

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa  Kilimanjaro Stars imetolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji Ethiopia baada ya  kucheza dakika 90 na kupata  sare ya bao 1-1.
 
Katika mchezo huo wa Robo Fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Kili Stars iliongoza kwa bao lililofungwa  na  John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kupata pasi ya Deus Kaseke dakika ya 25.

 
Ethiopia walisawazisha kipindi cha pili dk. 57 katika bao lililofungwa na  Panom Gathouch baada ya Mohammed Naser kuangushwa na  Shomary Kapombe

Waliokosa penalti ni Shomary Kapombe na  Jonas Mkude huku waliofunga ni Himid Mao, mshambuliaji Bocco na beki Hassan Kessy.

 
Waliofunga penalti za Ethiopia ni Panon Gathouch, Mohammed Naser, Ashalew Tamene na Behaylu Girima.  

 
Aidha,  Uganda imeifunga 2-0 Malawi mabao ya Farouk Miya na Ceasar Okhuti na sasa itakutana na Ethiopia katika Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment