| Mchezaji wa ngumi wa kike Salma Kihombwa wa Morogoro akilonga jambo katika mahojiano katika ukumbi wa Habari Maelezo. |
| Asha Ngedere akiwa katika pozi akimaanisha amejiandaa kumkabili mpinzani wake Salma. ili kujua nani zaidi ni siku hiyo ya April 28, mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba. |
Asha
Abobakari Nzowa 'Asha Ngedere' atamba kumpiga kipigo na mbwa mwizi mpinzani
wake kutoka Morogoro Salma Kihobwa katika pambano la ndondi April 28, mwaka huu.
Jina la Asha
Ngedere sio jina geni kwani ni maarufu kutokana na Zecomed kumtaja sana katika
vipindi vyao vya TBC.
Ni kijana
mdogo mwenye umri wa miaka 24 lakini mambo yake ni makubwa. Ili kujua nani
zaidi kati ya Asha Ngedere na Salma siku
hiyo inasubiriwa kwa hamu.
Kwa mujibu
wa Asha anasema kwanini uandikie mate wakati wino upo hivyo anahamasisha akina
dada kujitokeza na kuona nani zaidi.
Kwake Salma
mwenye umri wa miaka 17 anasema Asha bado mtoto atampiga hadi atambae kwa miguu. Hayo yote ni maneno tu
kinachosubiriwa ni siku hiyo.
Shindano
hilo limedhaminiwa na Kitwe General Traders.
No comments:
Post a Comment