Bondia wa
ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka ‘SMG’, wa Mji Kasoro Bahari Morogoro,
ametamba kutoa kipigo kikali kwa
mpinzani wake Mada Maugo ‘Mbunge wa Rorya’ wa jijini Dar es Salaam.
Cheka na Mada wanatarajiwa kuwania ubingwa wa IBF, uzito wa
Middle raundi 12, pambano litakalofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es
Salaam, ambapo limepangwa kufanyika Aprili 28 na kusimamiwa na Oganaizesheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Cheka
anasema kichapo kiko pale pale kwani amejiandaa vizuri na kwasababu yeye ni
bingwa hamwogopi Mada kwa vile aliwahi kumpiga mara 2 , na kumpiga Rashid
Matumla mara 4 hivyo haoni sababu ya kushindwa.
“Nitamchapa
Maugo katika raundi za awali tu, kwani najiandaa vilivyo ili nisiharibu rekodi
yangu kwa mwaka huu,” alisema Cheka.
Kwa upande
wake Mada Maugo alisema kwa sasa amejipanga na anaamini kuwa mkanda utakuwa ni
wake, hatokubali uende kwa Fransis Cheka.
Pia,
kutakuwepo na pambano la wanawake ambapo Asha Ngedere ametamba kumpiga kipigo
cha mbwa mwizi Salma Kihombwa wa Morogoro. Kila mmoja anatamba kummaliza
mwenzake.
Akizungumzia
kuhusu pambano hilo Promota wa pambano
hilo Lucas Rutainurwa alisema tayari mkanda umeshawasili kutoka Marekani
kinachosubiriwa kwa sasa ni pambano kwani kila kitu kimekamilika.
Mdhamini wa gari katika pambano hilo ambaye ni Moses
Katabaro wa kampuni ya Kitwe General Traders alisema gari ameshakabidhi lengo
ni kuhakikisha kuwa mchezo wa ngumi unachukuliwa kama ajira.
“Natoa
kipaumbele katika mchezo wa ngumi lengo ni kutambulisha mchezo huo ili hatimaye
wachezaji wauchukulie kama ajira muhimu kwao, gari tumekabidhi tunachosubiri ni
ushindi siku hiyo,”alisema.
No comments:
Post a Comment