Wengi
wanaonenaka kutokuwa na elimu ya kutosha ndio maana wanaendelewa kukandamizwa
na mfumo unaoendeshwa na Serikali.
Mada
iliyokuwa ikiendeshwa katika semina za GDSS ambazo hufanyika kila Jumatano
katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania ilikuwa ikisema ‘Historia ya
Uporaji Ardhi katika Muktadha wa katiba Tanzania’
Mtoa mada
katika semina hiyo alikuwa ni Dk. Ngwauza Kamata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam ambapo alisema mfumo uliopo umelenga kuwakandamiza watanzania bila kujua
kwani wengi hawana uelewa na kile kinachoendeshwa na serikali.
Serikali ya
Tanzania imekuwa ikitangaza ardhi ya Tanzania kwa wageni na kuwaacha watanzania
wengi wakiwa ni watu wa kutanga tanga kwani kila kukicha utasikia mgogoro wa
ardhi ya mwekezaji na wananchi.
Kwa mujibu
wa Dk. Kamata ni kwamba kwa sasa watu wengi kwa sasa wanalala nje kuliko miaka
ya 80. Kumekuwa na ongezeko la majengo marefu lakini mengi hujengwa kwa ajili
ya kukodisha ofisi na sio kwa ajili ya wananchi kukaa.
Lakini ili
wananchi waweze kufanya mapinduzi makubwa kutetea ardhi yao ili isiendelee
kuuzwa kiholela kwanza jambo la muhimu linasisitizwa na Dk. Kamata wananchi
kujiandaa na kujipanga kwa maana ya kuwa na umoja ili kudai haki zao.
Na kujipanga
huko sio tu kuzungumza kwa maneno bali kwa vitendo kama ambavyo nchi nyingine
zimekuwa zikifanya na kufanikiwa. Botswana ni moja ya nchi ambayo ilifanikiwa
kutetea ardhi yake.
Baadhi ya
wana GDSS wengine walisema kwanza umiliki wa ardhi kwa wananchi uingizwe kwenye
katiba mpya. Serikali isiendelee kuwapora wananchi ardhi yao na kuwaacha
wakitangatanga ndani ya nchi yao.
Lakini zaidi
wanasisitiza wanawake wapewe nafasi ya kumiliki ardhi.
No comments:
Post a Comment