KAMISHNA wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dunford Makala amewataka wadau wa utetezi wa watu wenye ulemavu kuendelea kushirikiana katika
kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu nchini.
Akizungumza katika mkutano wa ufunguzi wa wadau wa
utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu Kamishna Dunford Makala alisema Wizara
kupitia idara ya ustawi wa jamii imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya utoaji
huduma kwa watu wenye ulemavu na waishio katika makazi ya wasiojiweza, sambamba
na kuendeleza vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wenye ulemavu.
“Ushirikiano wetu wa hali na mali ndio utasaidia
kuboresha maisha na huduma kwa watu wenye ulemavu na wizara kupitia idara ya
ustawi wa jamii imeendeleza ushiriki wake kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili
ya huduma kwatu wenye ulemavu pamoja na kuendeleza vyuo vya ufundi stadi”
alisema.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na hayo changamoto
inayowakabili ni ufinyu wa bajeti inayotolewa na serikali kwa ajili ya huduma
hizo, pia alisema kanuni za sheria ya watu wenye ulemavu imesahapita katika
hatua zote za awali na sasa iko kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya mapitio.
Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Lupi Maswanya aliwashukuru
wadau kwa kuendelea kutoa ushirikiano wao wa hali na mali kwa kukubali na
kutambua ushirikianon wao.
No comments:
Post a Comment