TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday, 8 April 2012

Uzinduzi wa Kikundi cha Amani uliofanyika nyumbani kwa Mama Adam usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka

Kikundi cha Amani ambacho kimezinduliwa usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka kinajivunia kupata mafanikio  mbalimbali hasa ya kusaidiana katika matatizo yakiwemo wizi, harusi, magonjwa na matatizo mengine. Kilianza kma utani kwa kuchangishana fedha kwa ajili ya kusaidiana kwenye matatizo lakini leo wameamua kukiboresha kikundi chao ili kukopeshana kwa ajili ya maenedeleo mengine.
Tangu kianze kimetimiza mwaka mmoja lakini katika sherehe yao hiyo walifanya harambee kwa wadau na waume zao ambao walifika kushuhudia na kupata ahadi mbalimbali za kuboresha mfuko.

Mweyekiti wa Kikundi hicho Asteria Wilfred anasema lengo la kikundi chao ni kusaidia wanachama wote kwenye shida na raha, vile vile kuanzisha Saccos ambayo itawawezesha wanakikundi kukopa na kuanzisha miradi ya maendeleo.


No comments:

Post a Comment