TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 17 May 2012

Ally J awalaumu wanaomlaumu kuwa aliwatoa kafara five starsAlly J wa kwanza kushoto akizungumza jambo
 
RAIS wa kundi la Five Stars Modern Taarab, Ally Juma ‘Ally Jay’ amesema, anasikitika kuona kuwa kuna watu wanaoamini kwamba, amehusika kuwatoa kafara wasanii wenzie, kwenye ajali iliyolikumba kundi lao, Machi 21, mwaka jana.
 
Ally J, mahiri kwa upapasaji kinanda, aliyasema hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Shamsham za Pwani, kinachorushwa kila wiki, katika siku za Jumamosi, kwenye runinga ya ITV.   
 
“Unajua, kuna wengine hawaamini kuwa nami nilikuwamo kwenye gari iliyopata ajali siku ile, eti kwa sababu tu nilinusurika na kutoka bila jeraha,” alisikitika Ally Jay.
 
Alisema kuwa, ajali ile ni mipango ya Mwenyezi Mungu, ambako hata yeye aliguswa vilivyo na kuzidi kuumia kila anapowakumbuka wasanii wenzie waliopoteza maisha kwenye tukio hilo .
 
Aidha, Ally Jay aliiomba jamii kuachana na fikra potofu za kuhusisha matukio ya maafa na vifo vya wasanii na imani za kishirikina, ambako alisema kuwa hali hiyo husababisha migongano mikubwa.
 
Alisema, mara nyingi yanapozuka matukio ya namna hiyo, wanajamii huwa wepesi kukurupuka kutafuta mchawi, huku wakisahau kuwa kila jambo linapangwa na Mungu.
 


No comments:

Post a Comment