TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 17 May 2012

Dr. Mukangara kufunga fainali za mchezo wa bao Jumamosi


Dk.Fenella Mukangara
 Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dr. Fenela Mukangara anatarajiwa kufunga mashindano ya fainali za mchezo wa bao Jumamosi hii ambapo timu nne kati ya tisa zilizoshiriki mashindano hayo zilifanikiwa kutinga  fainali katika michuano ya mchezo hiyo.

Katika mashindano hayo ambayo yalianza rasmi April 26 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 48 ya Muungano jumla ya timu tisa zilishiriki ikiwa ni pamoja na Mlaponi, Mtea, Muungano, Nyayo na Kilamba, Uyaga, Kopa, FFU na Magereza.

Akizungumza na blogu hii kwa njia ya simu Rais  wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (Shimbata) Monday Likwepa alitaja timu nne zilizofanikiwa kutinga fainali kuwa ni pamoja na Mlaponi na Uyaga ambazo zinaoongoza zikifuatiwa na Kopa na Muungano.

“Tumeshapa timu nne zilizoingia fainali na tunategemea Jumamosi zitakapochuana ili kupata mshindi Dk. Mukangara atakuwa ndiye mgeni wetu atakayetoa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo,”alisema Likwepa.

Alisema mshindi wa kwanza anatarajiwa kunyakua kitita cha shilingi 400,000, wa pili 200,000 na wa tatu 100,000 wakati mshindi wan ne atanyakua 80,000. Pamoja na hao, mfungaji bora atanyakua 40,000, nidhamu ya bao 40,000, kamisaa bora 30,000 na kifuta jasho ni shilingi 20,000 kwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment