TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 28 May 2012

CHARS KUOA BAADA YA KUMALIZA NYUMBA YAKE


Rais wa bendi ya Mashujaa musica Chars Siprian ‘Chars Baba’ amesema anasubiri kumalizia kibanda chake ndipo amtambulishe mchumba wake mpya na kufunga naye ndoa.

Msanii huyo wa dansi ambaye aliwahi kutamba katika bendi ya Twanga Pepeta alisema kwa sasa hawezi kumtambulisha  hadi hapo atakapotimiza malengo yake hasa kumalizia nyumba yake.

Chars kwa sasa ni baba wa watoto wawili kwa mama tofauti huku mmoja akizaa na msanii mwenzake Sajenti Husna. Hata hivyo, alisema wameshaachana na Husna na tayari ni mchumba wa msanii wa dansi wa kundi la Mapacha.

Pamoja na hayo, alitambulisha wimbo mpya ambao Bendi ya Mashujaa imeuachia hivi karibuni unaojulikana kama Risasi kidole akimaanisha kuwa watu wengi wanapenda kuwanyooshea kidole wale ambao wameishiwa na kuwasema vibaya jambo ambalo sio zuri.

Hivyo wimbo ni elimu tosha dhidi ya wale wote wanaopenda kusema sema watu vibaya.

No comments:

Post a Comment