TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 28 May 2012

NASH AMEACHIA NGOMA MPYA


 

BAADA ya kutamba na wimbo wake wa ‘nasemwa semwa’  msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini wa THT,  Nash Dizaina  ameachia  ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Ujinga huo ambao ameutengeneza mwenyewe .

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nash alisema  wimbo huo tayari umeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na kwamba mashabiki wake waufuatilie ili wapate kuburudika.
 
"Nimefanya vizuri sana katika wimbo huo kutokana na ubunifu ambao nimeufanya hali inayoashiria naweza kurudi tena kwenye chati ya muziki wa bongo fleva kwa muda mrefu sasa," alisema Nash

Pia,  msanii huyo aliwaomba mashabiki wa muziki huo kumpa ushirikiano wa kutosha katika wimbo huo kwa kumuunga mkono hasa pale atakapokuwa katika shoo ambazo hupiga Maisha kila mwishoni mwa wiki.

Mbali na wimbo huo aliwahi pia kuvuma na wimbo wa 'No time' ambao aliimba remix ikiwa ni kopi kutoka kwa msanii wa Nigeria Brackets.

No comments:

Post a Comment