TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 18 May 2012

DIAMOND KUMSINDIKIZA OMMY DIMPOZI KATIKA UZINDUZI WA WIMBO MPYA WA BAADAYE



 Msanii  wa Bongo fleva nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kumsindikiza mzee wa Nai nai, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ wakati anatambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Baadae’.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Ommy alisema Baadae ni wimbo wake mpya ambao atautambulisha kwa mashabiki wake Jumapili ndani ya  ukumbi wa  Bilicanas uliopo Posta mpya jijini Dar es Salaam.
“Diamond namkubali sana ndio maana nimemuomba anisindikize kuitambilisha kazi yangu mpya ambayo najua mashabiki wangu wanaisubiri kwa hamu sana” alisema Ommy.
Alisema kazi hiyo ipo kwa upande wa audio peke yake na kwasasa anajipanga kwenda nchini Afrika Kusini kwaajili ya kufanya video ya wimbo huo.
Ommy ambaye alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliopata tuzo ya Kilimanjaro aliwaomba mashabiki waweze kufika kwa wingi katika shoo yake, na kutaka wasubiri mambo mazuri kutoka kwake kwani kuna mambo mengi aliyowaandalia.

No comments:

Post a Comment