TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 18 May 2012

SUMA LEE KAACHIA WIMBO MPYA WA UTAMKUMBUKA


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif ‘Suma Lee’ kaachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Utamkumbuka’ ambao kamshirikisha mtayarishaji wa muziki huo Khalifani Majani ‘P.Funk’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Suma Lee alisema wimbo huo katengeneza tofauti na nyimbo zake nyingine kwa lengo lakuwapa radha tofauti mashabiki wake.
“Wimbo naamini utafanya vizuri zaidi na mashabiki wangu wataupenda kupita kiasi hivo nawaomba wapenzi wangu waeendelee kunipa sapoti katika kazi zangu” alisema Suma Lee.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika Studio ya Bongo rekodi na imetengenezwa na watayarishaji mahiri pamoja na P.Funk mwenyewe.
Mbali na wimbo huo, Suma Lee alishawahi tamba na nyimbo zake kama Hakunaga, Chungwa na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na luninga.

No comments:

Post a Comment