Chama cha Judo Tanzania (JATA) kimempata mdhamini wake mkuu ambaye ni Yuliy Tarverdyan ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Gemini Corporation Ltd atakayedhamini
mashindano ya kitaifa ya mchezo huo
yatayotarajiwa kutimua vumbi Mei 26 na
27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama hicho Khalifa Kiumbemoto ‘Chief
Kiumbe’ alisema mfadhili huyo ni raia kutoka Urusi na ni mfadhili wa kwanza kujitokeza katika
Uongozi huo mpya ambao unaongozwa na
yeye.
Alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mashindano
hayo yatakuwa ni ya kwanza kufanyika
nchini ambapo zaidi ya wachezaji 100 kutoka Tanzania Bara na Visiwani
wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika katika Hotel ya
Landmark.
“Tunashukuru sana Kampuni hii kwa kujitokeza ili
kutuunga mkono, kwani ni fursa hii ni ya
kipee na haijawahi kutokea katika tasnia ya mchezo huu hapa nchini, tunaamini
kwamba mashindano ya kuwalipa washindi pesa itasaidia kukuza viwango,”alisema.
Alitaja zawadi kwa washindi kuwa mshindi wa kwanza
atapewa dola 600 kulingana na kilo, mshindi wa pili atapata dola 300, mshindi
wa tatu dola 100 pamoja na medali na cheti cha ngazi ya Diploma.
Naye Yuliy
tarvedyan ambaye ndiye mdhamini wa mashindano hayo alisema anatarajia
kutoa fedha zaidi ya dola 25,000 ikiwa
ni udhamini wake katika mashindano hayo.
Alisema kampuni yake ya Gemini imepanga kudhamini
mashindano ya kitaifa na kimataifa ya mchezo huo ili kuinua mchezo huo ili
hatimaye JATA iweze kufikia malengo yao
na kuwawezesha vijana wengi kuupenda mchezo huo.
“Tunaamini kwamba kutoa zawadi za fedha kwa wachezaji
kutaleta matokeo mazuri ya mchezo huo na kuwafanya wachezaji kujitahidi
kushindana kwani tunahitaji kupata wachezaji wazuri watakaoshindana kitaifa na
kimataifa,”alisema.
Tarvedyan alisema vifaa mbalimbali kwa Club zote
nchini kwa Tanzania bara na Visiwani kwa ajili ya kujiandaa na mchakato wa
mashindano.
No comments:
Post a Comment