TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 16 May 2012

SERENGETI YATANGAZA WASHINDI WENGINE WA PROMOSHENI YA ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL.



Zaidi ya watu 2007 wamejishindia zawadi mbalimbali ikiwemo bajaji, fedha, Jenereta baada ya kushinda katika promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)

Akiongea na Waandishi wa Habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya SBL Bi. Teddy Mapunda, alisema hadi sasa wameshapata washindi wawili wa jenereta ambapo tayari wamewakabidhi  zawadi zao, wengine ni washindi wa bajaj moja na wa pikipiki moja ambao nao wameshakabidhiwa zawadi zao.

Hata hivyo, zaidi ya milioni 780 zinashindaniwa katika promosheni hiyo. “Tunawashauri wateja wetu na watanzania wote wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii kwa wingi bila kukata tamaa na hatimaye nao waweze kushinda kwani promosheni yetu ni ya kweli, ya uhakika na ya haraka.”Alisema.

 Aliongeza kuwa  mpaka sasa tayari watu zaidi ya 2000 wamejishindia pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa hizo kwa urahisi kabisa kupitia mtandao wa kutuma na kupokea pesa wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom MPESA ndani ya masaa ishirini na nne. Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hiyo.

Washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali ni pamoja na Amadeus Minja na Agness Msengi wakazi wa Dar es salaam, walijishindia jenereta (kangavuke) kubwa ambapo walikabidhiwa zawadi hizo mwisho mwa wiki iliyopita. Ibrahim Kimambo mkazi wa tabata jijini Dar es salaam alibahatika kujinyakulia pikipiki mpya na ya kisasa ambapo naye alikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bw. Ibrahim ambaye hakuwa na kazi yoyote mpaka bahati iliyobebwa na promosheni hii ilipomdondokea  alikuwa na haya ya kusema, “kwa kweli nilipopata taarifa ya kushinda zawadi ya pikipiki sikuamini lakini sasa nimeamini na nawashukuru sana SBL kwa kuwa sasa naweza kujiajiri na kuendeleza maisha yangu na wale wanaonitegemea”. Kutoka jijini Mwanza Godfrey Shao ambaye alijinyakulia bajaj ya gurudumu tatu anaendelea kusubiri taratibu za usajili zikamilike ili aweze kukabidhiwa bajaj yake.

Aidha, kampuni hiyo iliendesha droo ya tatu leo na kupata washindi wengine ambao ni pamoja na   Fadhili Manzi mkazi wa Mafinga mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager ambaye amejishindia bajaj   na Raymond Denis mkazi wa Iringa ambaye  amejinyakulia jenereta kupitia bia ya Tusker Lager.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment