TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 4 May 2012

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi akiwaelekeza waandishi wa habari kwa njia ya vitendo

Mkuu wa Idara ya Utawala na Fedha Anna Kikwa na Afisa Programu Kenny Ngomuo wa RGNP wakiwaeleza jambo Waandishi wa Habari katika mafunzo hayo


Waandishi wa Habari wakifanya mafunzo kwa njia ya majadiliano


Waandishi wa Habari wakijadiliana

Waandishi wa Habari wamehimizwa kuandika na kuchambua mapungufu yalioko katika katiba ya sasa ili yaweze kuondolewa katika mchakato wa kuandaa katiba mpya  na kuingizwa yale yanayohitajika kwa manufaa ya watu wote.
Akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa TGNP Lilian Liundi alisema katiba iliyopo ina mapungufu mengi ambayo yanahitaji kuondolewa ili kuwanufaisha watu wote.
Alisema katiba hiyo bado haiwanufaishi wanawake walioko pembezoni hali inayoonyesha wazi kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuchambuliwa kwa kina ili mambo muhimu yanayowahusu wanawake yaweze kuingizwa.
Mwezeshaji mwingine katika mafunzo hayo Anna Kikwa aliyataja baadhi ya mapungufu yaliyoko katika katiba hiyo kuwa ni kutokuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali kwa maana ya madini, ardhi na nyingine.
Pia, akazungumzia umuhimu wa kuondolewa kwa hukumu ya kifo ambayo ni sawa na ukiukwaji wa haki za binadamu, Majukumu ya rais yapunguzwe, Waziri wasiwe wabunge , mgombea binafsi na masuala mengi ambayo bado yanahitaji kuchambuliwa kwa kina.
Mafunzo hayo ambayo ni ya siku tatu yameandaliwa na TGNP ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari jinsi ya kuweza kuandika habari za jinsia kwa uchambuzi.  
No comments:

Post a Comment