TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 11 May 2012

Wabunge kuchuana na Mabalozi kesho Karume


 
Timu ya mpira ya wabunge inatarajia kuchuana vikali na timu ya Umoja Ulaya kesho katika Viwanja vya Karume ikiwa ni sehemu ya kusherekea wiki ya Umoja wa Ulaya.

Pamoja na mechi hizo, pia kutakuwa na tamasha la filamu ambapo filamu 15 za kitanzania zitaoonyeshwa kwa kifupi kuanzia Mei 11 hadi  15 sehemu tofauti ikiwemo British Council, Goethe Institute na Alliance Franci.

Pia, kuna filamu nyingine 15 kutoka nchi za umoja wa Ulaya zitaonyeshwa katika sehemu zilizotajwa hapo juu. Ili kufahamu zaidi tembelea vituo vya filamu uone ratiba kamili ilivyo, lakini watakuwa wanaonyesha kuanzia saa moja usiku.

 Vile vile, Jumapili kutakuwa na Maandamano ya baiskeli kuanzia pale Mnazi mmoja hadi Biafra hivyo wale wanaopenda kusherekea na Umoja wa mataifa mnakaribishwa kwenda kuendesha baiskeli ili kusherekea pamoja wiki ya Umoja wa Ulaya. 

No comments:

Post a Comment