Na Mwandishi
wetu
Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii inawajulisha wasafiri wote wenye umri zaidi ya mwaka
mmoja wanatakiwa siku tisa kabla ya kuingia nchini Srilanka wawe wamepata
chanzo ya homa ya manjano.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Regina Kikuli
inaeleza kuwa utaratibu huo pia utahusisha wasafiri wanaopita nchini humo ambao
watakuwa wanasubiri usafiri wa kwenda nchi nyingine.
Utaratibu huo
umekuja kufuatia Wizara hiyo kupokea taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri kutoka
Tanzania kwenda Jamhuri ya Kisoshalisti ya Srilanka.
Kwa mujibu
wa Ubalozi wa Jamhuri ya Srilanka uliopo
Afrika ya Kusini unaeleza kuwa kila msafiri anayeingia Srilanka atatakiwa kuwa
na kadi ya chanjo ya homa ya manjano kama sharti la kiafya la kuingia nchini
humo madhumuni makubwa yakiwa ni kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa homa ya
manjano nchini humo.
Kwa wale
wasafiri ambao hawatastahili kuchanja chanjo hiyo kutokana na sababu za msingi
za kiafya kama vile wasafiri wenye umri chini ya mwaka mmoja, wazee wenye umri
zaidi ya miaka 60, wajawazito, waathirika wa virusi vya ukimwi na wenye
matatizo mengine ya kiafya watatakiwa kuonyesha uthibitisho kutoka kwa daktari.
No comments:
Post a Comment