Kongamano linalojulikana kama Global
Media Forum ambalo linawaleta pamoja wataalamu kutoka vyombo vya habari,
wanasayansi na wanasiasa, limeanza leo Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika jengo
la Deutsche Welle mjini Bonn
" Elimu bado ni mada kuu katika
suala zima la utandawazi," alitamka hayo Mkurugenzi mkuu wa Deutsche
Welle, Erik Bettermann. Jinsi gani " Elimu kwa wote" lilivyo jambo
muhimu, ndiyo suala kuu la majadiliano ya siku tatu miongoni mwa wataalamu
kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa kuanzia Jumatatu (Juni 25
hadi 27 ) katika kongamano linalojulikana kama Global Media Forum katika jengo
la Deutsche Welle mjini Bonn." Habari na elimu ndiyo msingi wa harakati za
chombo cha matangazo ya kigeni cha Ujerumani", anasema Mhariri mkuu wa DW,
Ute Schaeffer.
Kwa mujibu wa idadi rasmi ya Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa, kiasi ya watu 800 milioni
hawajui kusoma na kuandika.Wakati huo huo, inaelekea Ulimwengu ni jamii ya
habari, ambayo kwa mujibu wa Erik Bettermann,hutupa nafasi ya kupata maarifa
kila wakati na popote tulipo.
Vyombo vya habari kutoa mwangaza
Ni kwa sababu hii hasa, vyombo vya
habari kote duniani vinawajibu. " Vina jukumu muhimu kama chombo cha kutoa
muwangaza ", anasisitiza Mkurugenzi mkuu wa DW. Kwa watu wa tabaka mbali
mbali katika Dunia ya utandawazi, elimu, utamaduni na elimu kwa wote, yanaweza
kuwa ni ufunguo wa kuweza kuishi pamoja kwa amani, kwa maendeleo na majadiliano
baina ya watu wa tamaduni mbali mbali.
Katibu mkuu wa Tume ya Ujerumani ya
Shirika la UNESCO , anakubaliana na msimamo huu:" Uhuru wa magazeti, ubora
wa elimu na mchanganyiko wa tamaduni, ni mambo muhimu kwa ajili ya kuwa na
jumuiya huru na zenye nguvu. Mwaka huu Tume ya Ujerumani ya Shirika la
UNESCO,imechukua nafasi ya kuwa kinara ya mkutano wa Bonn.
Miongoni mwa wageni maarufu katika
kongamano la Global Media Forum kawa mara ya kwanza ni Waziri wa mambo ya nchi
za nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle. Anazungumzia juu mchango wa ushirikiano
na maajadiliano katika Dunia ya utandawazi. Pia anatarajiwa Rais wa zamani wa
Indonesia Jusuf Habibie.
Misimamo ya Sayansi duniani
Thomas Pogge, profesa wa falsafa ya
siasa na masuala ya kimataifa katika chuo kikuu cha Yale, New Haven (Marekani)
na Franz Josef Radermachaer, profesa wa sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu
cha Ulm na mwanachama wa kilabu ya Roma, wataelezea wazi misimamo ya sayansi
katika hali ya dunia na hivyo kuwasilisha maelezo ya kutosha kwa ajili ya
majadiliano.
Lakini zaidi ya watu wengine 50
katika hafla hiyo-walioandaliwa na mashirika na makampuni ya kitaifa na
kimataifa , watatoa maoni mengi tofauti: UNESCO imetambuwa kuwa mchanganyiko wa
tamaduni ni chachu kwa hali endelevu katika kanda ya Ulimwengu wa Kiarabu.
Shirika la Ujerumani la
kubadilishana wasomi (DAAD), linajishughulisha na suala la kama vyuo vikuu
vinaweza kuwa chombo cha mabadiliko. Elimu ya haki za binaadamu na maamuzi
binafsi ya kijinsia ni mada inayozingatiwa na taasisi ya Ujerumani ya haki za
binaadamu (DIMR) na Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa (GIC) na Taasisi ya
Maendeleo ya Ujerumani (DIE), zinafafanua juu ya mchango wa mdahalo baina ya
tamaduni mbali mbali kwa changamoto za " utawala bora".
"Kwa hiyo sisi si mkutano wa
vyombo vya habari si mkutano wa kisiasa wala mkutano wa kisayansi,"
anasema Meneja wa GMF Ralf Nolting, bali ni watu tuliokusanyika katika meza
moja , kutathmini nini suluhisho la matatizo ya dunia." Kinachofaanana
kwetu sote ni imani ya kwamba vyombo vya habari vimetoa mchango muhimu katika
kutambua suluhisho la matatizo na mawasiliano.
Kutokana na hayo ndiyo maana kuna
Kongamano hili la Global Media Forum- ambalo sasa linafanyika kwa mara ya tano-
likiwa ni jambo la mafanikio , anasema Nolting.
Chanzo cha habari kwa hisani ya Swahilivilla
No comments:
Post a Comment