Na.
Luppy Kung’alo, Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la
Polisi Mkoa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel s/o
Lusega miaka (42) kabila mkaguru na mkazi wa Morisheni kata, tarafa na wilaya
ya kongwa kwa tuhuma za kumchinja mke wake na kumuua.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw.
ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo limetokea tarehe 25/06/2012 muda (08:00hrs)
wa saa mbili asubuhi leo, katika eneo la Morisheni Kata, Tarafa na Wilaya ya
Kongwa.
“Mtuhumiwa
alikwenda kuripoti mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kongwa kuwa
amemchinja na kumuua mke wake kwa sababu hamsikilizi.” alieleza Kamanda
Zelothe.
Bw, Zelothe
alisema mtuhumiwa huyo wakati anaripoti tukio hilo katika kituo cha Polisi
alikuwa na barua mkononi ikieleza madai hayo kwa marehemu mke wake, ikiwa na
anuani ikielekeza kwa Afisa Usalama wa wilaya ya Kongwa, lakini barua hiyo
ameikabidhi katika kituo cha Polisi.
Kamanda ZELOTHE
STEPHEN alimtaja mwanamke huyo aliyeuwawa kuwa ni Telophena w/o Machimo umri
miaka (34) kabila Mkaguru, muuza mgahawa na Mkazi wa Morisheni wilayani
kongwa
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema
askari walikwenda kukagua eneo la tukio na kukuta marehemu amechinjwa kwa
kukatwa koromeo na akiwa katika dimbwi la damu pamoja na kisu kilichotumika
kikiwa kando yake.
Kamanda huyo wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododma alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa
mapenzi kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kwa kutembea nje ya ndoa
pia kwa kutoleta matumizi ili hali merehemu ni muuza mgahawa katika eneo hilo
Hata hivyo
Kamanda Zelothe alisema mtuhumiwa huyo ana historia ya ugonjwa wa akili kwa
mujibu wa maelezo ya wanandugu na viongozi wa kijiji wa eneo hilo.
Mtuhumiwa
amekamatwa na anashikiliwa katika kituo cha Polisi Wilayani Kongwa na
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili, alisema Bw. Zelothe.
No comments:
Post a Comment