TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 15 June 2012

Mfanyabiashara apandishwa kizimbani kwa wizi


Na mwandishi wetu

MFANYABIASHARA Adam Karista (21) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka ya kutumia kisu kuiba mali zenye thamani ya Sh Sh 800,000.

Karista alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Ester Mwakalinga.

Wakili wa Serikali Naima Mwanga alidai kuwa, Desemba 9 mwaka jana katika eneo la Buguruni Kisiwani, Karista na wenzake ambao bado hawajafikishwa mahakamani walipanga njama na kuiba mali mbalimbali zenye thamani hiyo.

Naima aliendelea kudai kuwa, kabla ya kuiba mali hizo , Karista alitumia panga kumtishia John ili achukue mali hizo bila kipingamizi.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha haina dhamana.

Katika hatua nyingine, Mohamed Abas (40) amefikishwa katika Mahakama hiyo kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Serikali Aidah Kisumo alidai mbele ya Hakimu Tarsila Kisoka kuwa Aprili 28 mwaka huu saa 5:00 katika mtaa wa Uhuru, Abas alijipatia Sh milioni 12 kutoka kwa Kunambi Hamisi kwa madai ya kumrudia lakini hakufanya hivyo.

Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa rumande hadi Juni 28 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment